THIERRY Manzi raia wa Rwanda anatajwa kuwa kwenye hesabu za mabosi wa Simba kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo msimu ujao.
Simba imepishana na ubingwa ambao upo mikononi mwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia.
Yanga pia imetinga hatua ya fainali ya Azam Sports Federation iliposhinda mbele ya Singida Big Stars na inatarajia kucheza mchezo wa fainali Kombe la Shiriisho Afrika.
Kutokana na Simba kukwama kufikia malengo yao wapo kwenye mpango wa kuboresha kikosi hicho kwa msimu ujao.
Nyota huyo ambaye anapata namba kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda aliwahi kufanya kazi na Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira.
Ni katika Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda amewahi kucheza pia FA Rabat na AS Kigali.
Taarifa zinaeleza kuwa Simba ipo kwenye mpango wa kuachana na mabeki wake wawili ambao ni Joash Onyango na Mohamed Outtara ambaye huyu hajafiti kabisa kwenye mfumo wa timu hiyo.