YANGA HESABU KWENYE FAINALI KIMATAIFA

BAADA ya kukamilisha mchezo wao wa hatua ya nusu fainali ya Azam Sports Federation msafara wa Yanga umerejea salama Dar wakianza hesabu kwenye mchezo wao wa kimataifa.

Ni Mei 21 kikosi kilikuwa Uwanja wa Liti, Singida na ubao ulisoma Singida Big Stars 0-1 Yanga.

Bao pekee la ushindi lilipachikwa kimiani na Fiston Mayele ambaye aliingia akitokea benchi akichukua nafasi ya Aziz KI.

Ni Metacha Mnata alishuhudia mshikaji wake Benedict Haule akitunguliwa bao moja katika mchezo huo.

Mchezo wake ujao ni wa fainali ya kwanza dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mchezo ujao ni dhidi ya USM Alger ambao ni fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika huku ahadi ya bao la mama ikiwa ni milioni 20.