Home Sports DARASA LA YANGA KIMATAIFA NI KWA WOTE

DARASA LA YANGA KIMATAIFA NI KWA WOTE

KASI ya Yanga kwenye mashindano ya kimataifa ni darasa huru kwa kila mmoja apate kujifunza namna ya kutumia bahati na nafasi inayotokea.

Hakuna timu ambayo haipendi kupiga hatua kila siku na kuandika rekodi mpya na nzuri hilo lipo wazi hivyo kwa sasa mfano bora wa kuzungumzia kwenye kizazi cha sasa ni Yanga.

Mfumo ambao wameutumia umejibu na mbinu ambazo wametumia zimejibu kwa kuangalia makosa ya wapinzani na kutumia nafasi hiyo.

Katika kufika hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika huwezi kuweka wazi kwamba ni bahati mbaya ama imetokea ghafla hapana mipango kwenye kila hatua.

Waligundua wamekwama kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wakarejea kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho wakiwa na hasira ya kuandika rekodi mpya na makubaliano ya kufanya vizuri kila mchezo.

Hakika wameandika rekodi nzuri ugenini na nyumbani na sasa wapo kwenye hatua ya fainali nin tena wanahitaji wachezaji zaidi ya kupambana na kuleta taji kubwa la Afrika.

Huwezi kuiweka kando Simba kwenye soka la Afrika kutokana na kasi yao lakini wao hawajafikia hatua ya nusu fainali wala fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika hivyo ni muhimu kuungana na Yanga kwenye mchezo wa fainali.

Azam FC, Namungo, Singida Big Stars, JKT Tanzania, Ihefu pamoja na timu zote Bongo ni muda wa kuendelea kufuata yale mazuri na kuungana kutimiza kazi moja ya kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.

Previous articleMAYELE ATIKISA AFRIKA,MBRAZIL SIMBA ATANGAZA BALAA ZITO
Next articleSINGIDA BIG STARS YAIPIGIA HESABU YANGA