Home Sports SIMBA YAIPA NGUVU NAMUNGO

SIMBA YAIPA NGUVU NAMUNGO

KOCHA Mkuu wa Namungo, Dennis Kitambi amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Simba umewapa nguvu ya kufanya vizuri kwenye mechi ambazo zimebakia.

Namungo ilipokutana na Simba kwenye mchezo wa ligi ilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 mchezo wake dhidi ya Azam FC ilishinda mabao 2-1.

 Kitambi amesema kuwa wachezaji baada ya kucheza mchezo dhidi ya Simba walionyesha kiwango kikubwa jambo alilowaambia wanapaswa kuwa nalo mechi zote.

“Mchezo wetu dhidi ya Simba wachezaji walionyesha kiwango kikubwa licha ya kwamba hatukushinda lakini kuna kitu kilionekana niliwapongeza.

“Baada ya mchezo ule niliwaambia kwamba wanapaswa kuwa kwenye mwendelezo uleule kwa kiwango kile na hilo limeonekana kwenye mchezo wetu dhidi ya Azam FC tukapata ushindi hivyo tunaamini kwenye mechi zilizobaki tutaendelea na kasi yetu,” amesema.

Namungo imefikisha pointi 39 ikiwa nafasi ya tano kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 28.

Previous articleCHAMA, SAIDO MVURUGANO MTUPU SIMBA
Next articlePOLISI TANZANIA YAGOMEA KUSHUKA DARAJA