Home Sports CHAMA, SAIDO MVURUGANO MTUPU SIMBA

CHAMA, SAIDO MVURUGANO MTUPU SIMBA

MASTAA wawili ndani ya kikosi cha Simba, Saido Ntibanzokiza na Clatous Chama ni mvurugano mtupu kwenye kutengeneza pasi za mwisho ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

Yanga ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara wao mtambo wao wa mabao ni Fiston Mayele mwenye mabao 16 kibindoni.

 Wakati Chama ambaye ni kinara wa kutenegenza pasi za mwisho akiwa nazo 14 akiwa amegotea hapo kasi ya Ntibanzokiza ni moto kwa kuwa kwenye mechi mbili mfululizo za ligi ametoa pasi za mabao.

Ilikuwa mchezo dhidi ya Namungo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa alipotoa pasi moja ya bao na kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting alipotoa pasi mbili za mabao.

Jumla Ntibanzokiza katoa pasi 12 za mabao akibakisha pasi mbili kumfikia mshikaji wake Chama ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Roerto Oliveira.

Ikumbukwe kwamba mara ya mwisho kwa Chama kutoa pasi ya bao ilikuwa ni Februari 3,2023 alipotoa pasi mbili dhidi ya Singida Big Stars.

Kwenye mchezo huo Chama alitoa pasi mbili kwa mapigo ya faulo na moja kati ya pasi yake ya bao ilitumika na mshikaji wake Ntibanzokiza.

Licha ya orodha ndefu ya pasi walizonazo kibindoni mastaa hao wawili kikosi cha Simba kimegotea nafasi ya pili na pointi 67 kinara ni Yanga aliyetwa taji la ligi akiwa na pointi 74.

Timu zote zimecheza mechi 28 ni mechi mbili kwenye mikono yao zimebaki ambazo zitaamua nani atakuwa nani kwenye mpango kazi wa kutengeneza pasi za mwisho.

Previous articleYANGA: NINI MWARABU? TUNALITAKA KOMBE, BALEKE AFUNGUKA
Next articleSIMBA YAIPA NGUVU NAMUNGO