Home Sports YANGA BINGWA TENA

YANGA BINGWA TENA

BAADA ya kupata ushindi leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara rasmi Yanga wanakuwa ni mabingwa wa NBC Premier League.

Unakuwa ni ubingwa wa 29 tangu kuanzishwa kwake ikiwa ni historia kubwa na nzuri kwa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi,

Yanga wamefikisha pointi 74 ambazo hamna timu yeyote inaweza kufikisha ni baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 ambapo watupiaji kwa Yanga ni Kennedy Musonda, Mudathiri Yahya alitupia mawili na Farid Mussa alitupia bao moja.

Kwa Dodoma Jiji ni Collins Opare na Seif Karihe hawa walimtungua Metacha Mnata ambaye alianza langoni.

Previous articleKOCHA JULIO KAANZA MIKWARA
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE SPOTI XTRA JUMAPILI