Home Sports RUVU SHOOTING YAMUOMBA MUNGU KWENYE MAPITO YAO

RUVU SHOOTING YAMUOMBA MUNGU KWENYE MAPITO YAO

UONGOZI wa Ruvu Shooting umeweka wazi kuwa kwenye mapito magumu wanayopitia njia itaonekana.

Timu hiyo leo inatarajiwa kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Simba Uwanja wa Azam Complex kusaka pointi tatu.

Ikumbukwe kwamba vinara wa ligi ni Yanga wenye pointi 71 kibindoni baada ya kucheza mechi 27 msimu wa 2022/23.

 Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa wanamechi ngumu ambazo zimebaki wanamuomba Mungu wapite salama.

“Kweli ukitazama mechi ambazo zimebaki ni ngumu nasi tunamuomba Mungu tufanye vizuri na tutapita kwenye hizo mechi ngumu.

“Kuhusu kucheza wachezaji wanajituma na matokeo ya uwanjani huwa yanakuwa tofauti hivyo tunawaomba mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi bila kusahau kutuombea,” amesema.

Nafasi ya 16 ipo Ruvu Shooting baada ya kucheza mechi 27 ina pointi 20, Simba ipo nafasi ya pili na pointi 64.

Previous articleLIGI KUU BARA KINAWAKA LEO
Next articleHAPA NDIPO ANGUKO LA SIMBA LILIPOANZIA