Home Sports LIGI KUU BARA KINAWAKA LEO

LIGI KUU BARA KINAWAKA LEO

LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo Mei 12 ikiwa ni mzunguko wa pili.

KMC chini ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio” itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Singida Big Stars.

Ni Uwanja wa Uhuru ngoma inatarajiwa kupigwa ambapo KMC itawakaribisha Singida Big Stars saa 10:00 jioni.

KMC inapambana kubaki ndani ya ligi ikiwa imecheza mechi 27 na kuvuna pointi 26 ikiwa nafasi ya 14 inakutana na Singida Big Stars iliyo nafasi ya nne na pointi 51.

Mbali na mchezo huo, Simba iliyo nafasi ya pili na pointi 64 itawakaribisha Ruvu Shooting iliyo nafasi ya 16 na pointi 20, Uwanja wa Azam Complex saa 1: 00 usiku.

Previous articleVYUMA VITATU CAF MIKONONI MWA YANGA, ISHU YA CHAMA KUSEPA SIMBA
Next articleRUVU SHOOTING YAMUOMBA MUNGU KWENYE MAPITO YAO