Home International ILIKUWA KAZIKAZI AZAM FC V SIMBA NANGWANDA

ILIKUWA KAZIKAZI AZAM FC V SIMBA NANGWANDA

HAMNA namna ilikuwa ni lazima mshindani apatikane ndani ya dakika 90 kila shabiki anarejea na alichokivuna kutoka kwa timu yake.

Wale wa Simba ni safari ndefu kutoka Uwanja wa Nangwanda Sijaona mpaka kule wanakoelekea labda iwe ni Njombe ama Dar lakini wa Azam FC ni burudani tosha.

Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi wa taji hilo ni Yanga ambao watacheza na Singida Big Stars.

Mshindi wa mchezo atakutana na Azam FC kwenye hatua ya fainali.

Ubao ulisoma Azam FC 2-1 Simba hatua ya nusu fainali na mshindi anamsubiri atakayeshinda mchezo wa Singida Big Stars v Yanga Uwanja wa Liti hapa  tunakuletea namna kazi ilivyokuwa kwa kila mmoja kubeba mzigo wake:-

Iddrisu Abdulai

Kipa wa Azam FC alianza kikosi cha kwanza alitunguliwa bao moja dakika ya 27 na aliokoa hatari dakika ya 24,45,53,58, alipiga pasi ndefu dakika ya 32,38,58,65.
Lusajo Mwaikenda

Mwaikenda alifunga ukurasa kwa kufunga bao dakika ya 22 alipiga krosi dakika ya 10 alirusha dakika ya 11 aliokoa hatari dakika ya 35.
Bruce Kangwa

Daniel Amoah
Nyota huyu alichezewa faulo dakika ya 44,65,73 alipiga faulo dakika ya 25,74 aliokoa hatari dakika ya 41.
Abdalah Kheri
Nyota huyu aliokoa hatari dakika ya 12,41,77.

Ayoub Lyanga
Alipiga kona dakika ya 11,49,57,58 aliokoa dakika ya 16,30 alicheza faulo dakika ya 63 alirisha dakika ya 15 alipiga faulo dakika ya 22,

Bajana

Sospeter Bajana nyota wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano dakika ya 19 alicheza pia faulo dakika ya 52,alipiga krosi dakika ya 10,15 alichezewa faulo dakika ya 71 alipiga faulo dakika ya 61.

Idris Mbombo
Nyota huyu alipga krosi dakika ya 11 shuti ambalo lililenga lango dakika ya 12 alichezewa faulo dakika ya 12,43,49 alisepa na dakika 69 aliingia Prince Dube aliyefunga bao dakika ya 74 alipiga shuti lingine ambalo lililenga lango dakika ya 73 na aliokoa hatari dakika ya 84.

James Akamiko
Kiungo huyu wa Azam FC alipiga krosi dakika ya 9,53,69 alichezewa faulo dakika ya 61,85 alicheza faulo dakika ya 36,38,59.
Sopu

Abdul Seleman, aliokoa hatari dakika ya 41 alipiga krosi dakika ya 35 alichezewa faulo dakika ya 28.

Ally Salim

Kipa namba tatu wa Simba alitunguliwa mabao mawili, aliokoa hatari dakika ya 9,15,22,36,40,42,49,61,73.

 Shomari Kapombe

Alicheza faulo dakika ya 21, 65 aliokoa dakika ya 10 alipiga krosi dakika ya 32,39 alipiga faulo dakika ya 83.

Mohamed Hussein

Aliokoa hatari dakika ya 12.65 alipewa majukumu ya kurusha dakika ya 62 alipiga krosi dakika ya 31.

Joash Onyango

Aliokoa hatari dakika ya 24,29,36,42,60.

Henock Inonga

Aliokoa hatari dakika ya 10,23,31,59 alichezewa faulo dakika ya 62.

Sadio Kanoute

Alipachika bao moja dakika ya 27 alicheza faulo dakika ya 19,71,85 alionyeshwa kadi mbili za njano dakika ya 71 na 85 akaonyeshwa kadi nyekundu kiungo huy ambaye pia dakika ya 16 alipiga shuti ambalo halikuelnga lango.

 Clatous Chama

Alicheza faulo dakika ya 19,29,31, alichezewa faulo dakika ya 38,39 alipia shuti ambalo lililenga lango dakika ya 45.

Mzamiru Yassin

Alicheza faulo dakika ya 12,61,68 alichezewa faulo dakika ya 36,62.

Jean Baleke

Alipiga krosi dakika ya 15,41 alipiga shuti ambalo halikuelnga lango dakika ya 53 alisepa na dakika 81 aliingia John Bocco.

Ntibanzokiza

Saido Ntibanzokiza alipiga faulo dakika ya 27 alicheza faulo dakika ya 65.

 Kibu Dennis

Alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 15,64 alipiga krosi dakika ya 15,41 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 33 alisepa na dakika 81 aliingia Pape Sakho.

Previous articleKOCHA ONGALA KAWAZIDI SIMBA NJE NDANI
Next articlePANGA ZITO LAPITA SIMBA, BEKI LA CAF LASAINI YANGA