HAMNA namna ilikuwa ni lazima mshindani apatikane ndani ya dakika 90 kila shabiki anarejea na alichokivuna kutoka kwa timu yake.
Wale wa Simba ni safari ndefu kutoka Uwanja wa Nangwanda Sijaona mpaka kule wanakoelekea labda iwe ni Njombe ama Dar lakini wa Azam FC ni burudani tosha.
Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi wa taji hilo ni Yanga ambao watacheza na Singida Big Stars.
Mshindi wa mchezo atakutana na Azam FC kwenye hatua ya fainali.
Ubao ulisoma Azam FC 2-1 Simba hatua ya nusu fainali na mshindi anamsubiri atakayeshinda mchezo wa Singida Big Stars v Yanga Uwanja wa Liti hapa tunakuletea namna kazi ilivyokuwa kwa kila mmoja kubeba mzigo wake:-
Iddrisu Abdulai
Kipa wa Azam FC alianza kikosi cha kwanza alitunguliwa bao moja dakika ya 27 na aliokoa hatari dakika ya 24,45,53,58, alipiga pasi ndefu dakika ya 32,38,58,65.
Lusajo Mwaikenda
Mwaikenda alifunga ukurasa kwa kufunga bao dakika ya 22 alipiga krosi dakika ya 10 alirusha dakika ya 11 aliokoa hatari dakika ya 35.
Bruce Kangwa
Daniel Amoah
Nyota huyu alichezewa faulo dakika ya 44,65,73 alipiga faulo dakika ya 25,74 aliokoa hatari dakika ya 41.
Abdalah Kheri
Nyota huyu aliokoa hatari dakika ya 12,41,77.
Ayoub Lyanga
Alipiga kona dakika ya 11,49,57,58 aliokoa dakika ya 16,30 alicheza faulo dakika ya 63 alirisha dakika ya 15 alipiga faulo dakika ya 22,
Bajana
Sospeter Bajana nyota wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano dakika ya 19 alicheza pia faulo dakika ya 52,alipiga krosi dakika ya 10,15 alichezewa faulo dakika ya 71 alipiga faulo dakika ya 61.
Idris Mbombo
Nyota huyu alipga krosi dakika ya 11 shuti ambalo lililenga lango dakika ya 12 alichezewa faulo dakika ya 12,43,49 alisepa na dakika 69 aliingia Prince Dube aliyefunga bao dakika ya 74 alipiga shuti lingine ambalo lililenga lango dakika ya 73 na aliokoa hatari dakika ya 84.