Home Sports SINGIDA BIG STARS 0-2 YANGA

SINGIDA BIG STARS 0-2 YANGA

UBAO wa Uwanja wa Liti unasoma Singida Big Stars 0-2 Yanga ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara, mzunguko wa pili.

Singida Big Stars imeshuhudia mabao yakifungwa kipindi cha kwanza cha mchezo huo ambao unafuatiliwa na mashabiki wengi duniani.

Ni Aziz KI alipachika bao la kwanza kwa shuti kali ambalo lilimpoteza mlinda mlango Benedickt Haule na kazi ya pili ikiwa ni Clement Mzize.

Kiungo Bruno Gomes jitihada zake za kupachika mabao zinakutana na kizingiti cha mdaka mishale Djigui Diarra.

Previous articleMWAMBA WA LUSAKA NGOMA NZITO MSIMBAZI
Next articleZAMA ZA AZAM FC NA SIMBA ZILIKUWA NGUMU