>

SIMBA NDANI YA RUANGWA, LEGEN MKUDE NDANI

JONAS Mkude ni miongoni mwa mastaa wa Simba ambao wapo kwenye msafara ulipo Ruangwa,Lindi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo.

Mkude alikosekana kwenye mechi za hivi karibuni katika Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Simba ikifungashiwa virago na Wydad Casablanca hatua ya robo fainali kuanzia ule wa nyumbani hata ugenini.

Yupo kwenye kikosi Ruangwa kwa ajili ya mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Mei 3,Uwanja wa Majaliwa ukiwa ni wa mzunguko wa pili.

Kikosi hicho chini ya Kocha Mkuu Robert Oliviera kipo nafasi ya pili na pointi zake ni 63 vinara ni Yanga wenye pointi 68.

Wanakutana na Namungo iliyo nafasi ya 6 pointi zao ni 35 zote zimecheza mechi 26.