Home Sports MTAMBO WA MABAO YANGA WATOA NENO

MTAMBO WA MABAO YANGA WATOA NENO

MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ameweka wazi kuwa kazi kubwa ni kusaka ushindi katika mechi zao.

Ni Fiston Mayele mwenye mabao 16 ndani ya ligi na mabao matano katika Kombe la Shirikisho Afrika ametupia mabao matano kuanzia hatua ya makundi mpaka robo fainali.

Mei Mosi kikosi cha Yanga kilikwama safari ya kuelekea Singida kwa ajili ya maandalizi ya mwisho dhidi ya Singida Big Stars mchezo unaotarajiwa kuchezwa Mei 4 ambao ni wa Ligi.

Sababu ilikuwa ni ndege waliyokuwa wakisafiria kushindwa kutua Uwanja wa Ndege Dodoma lakini wachezaji wote wapo salama pamoja na benchi la ufundi.

Mayele amesema:”Tuna kazi kubwa kwenye mechi ambazo tunafanya na tunajua kwamba ushindani ni mkubwa jambo amalo linafanya nasi tufanye maandalizi mazuri.

“Kikubwa ni kupata matokeo na tunaamini inawezekana kwa kuwa sisi ni timu moja na benchi la ufundi linatupa mbinu ambazo zinatupata matokeo chanya,”.

Kwenye mchezo wa mzunguko  wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Yanga ilisepa na pointi tatu na Mayele alitupia hat trick ya kwanza na pasi yake ya kwanza ndani ya ligi msimu wa 2022/23.

Previous articleSIMBA NDANI YA RUANGWA, LEGEN MKUDE NDANI
Next articleKIUNGO RIVERS UNITED AKUBALI KUTUA YANGA