MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ameweka wazi kuwa kazi kubwa ni kusaka ushindi katika mechi zao.
Ni Fiston Mayele mwenye mabao 16 ndani ya ligi na mabao matano katika Kombe la Shirikisho Afrika ametupia mabao matano kuanzia hatua ya makundi mpaka robo fainali.
Mei Mosi kikosi cha Yanga kilikwama safari ya kuelekea Singida kwa ajili ya maandalizi ya mwisho dhidi ya Singida Big Stars mchezo unaotarajiwa kuchezwa Mei 4 ambao ni wa Ligi.
Sababu ilikuwa ni ndege waliyokuwa wakisafiria kushindwa kutua Uwanja wa Ndege Dodoma lakini wachezaji wote wapo salama pamoja na benchi la ufundi.