HAITAKUWA MWISHO MPAKA IGOTE MWISHO

HAITAKUWA mwisho mpaka ifike mwisho kwenye mashindano yote ambayo timu zinashiriki iwe ni kwenye ligi ama Kombe la Shirikisho.

Ipo wazi kwamba bingwa mtetezi wa mataji yote ni Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Yanga wao watakutana na Singida Big Stars mchezo wa hatua ya nusu fainali na Azam FC watamenyana na Simba kweye Kombe la Shirikisho.

Kwa sasa tunaona kuna timu ambazo zimeshatambua wapi zitakuwa msimu ujao lakini kuna mechi ambazo wanazo mkononi hizi zinawahusu lazima wacheza.

Zipo pia ambazo zina mechi kwenye Kombe la Shirikisho ikiwa ni hatua ya nusu fainali hakika kazi bado ni ngumu kwenye dakika 90 za kusaka ushindi.

Ambacho kinatakiwa ni umakini na maandalizi mazuri kwenye mechi zote bila kujali aina ya mashindano husika.

Muhimu ni kupata matokeo baada ya dakika 90 na haya hayajitokezi bure ni lazima kupambana bila kuchoka na kufanya maandalizi mazuri.

Msingi mkubwa unajengwa kwenye nidhamu nje na ndani ya uwanja na hili litawafanya wachezaji kuonyesha upekee wao kwenye kukamilisha safari ya mwisho.

Hakuna ambaye hapendi kuona timu inapata matokeo lakini kikubwa ni kujipanga kwa umakini nakutumia nafasi ambazo zinapatikana kwenye mechi husika.

Mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa ambacho kinahitajika kwa timu ambayo inahitaji ushindi ni kuwa makini kwenye kupunguza makosa.

Jambo lingine muhimu ni afya za wachezaji kwa kulindana ndani ya uwanja wakati huu wa ligi kugota mwisho.

Imekuwa ni kasumba ya wachezaji wengi kupenda kutumia nguvu kubwa wakati huu wa lala salama hii sio sawa ni muhimu kila mchezaji kuwa makini.