UBAO wa Uwanja wa Mohamed V unasoma Wydad 1-0 Simba.
Safu ya ulinzi ya Simba imekwama kuwazuia Wydad Casablanca kwa kusababisha kosa la kona ambalo limeigharimu timu hiyo.
Junior Boll kaonyesha ukomavu wake mbele ya ukuta wa Simba na kupachika bao la kuongoza dakika ya 23.
Huu ni mchezo wa maamuzi utakaotoa picha nani atasonga mbele hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.