WASHIKA BUNDUKI MAMO MAGUMU, CITY WAPIGA 4G

MANCHESTER City wakiwa Uwanja wa Etihad walibaki na pointi zote tatu muhimu dhidi ya Arsenal.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Manchester City 4-1 Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Kevin De Bruyne alipachika mabao mawili dakika ya 7,54 huku John Stones alipachika bao moja dakika ya 45 na msumari wa nne Mali ya Erling Haaland.

Kwa washika bunduki ni bao la jioni mtupiaji Rob Holding dakika ya 86 katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

City inafikisha pointi 73 imecheza mechi 31 ikiwa na mechi mbili mkononi na Arsenal pointi 75 nafasi ya Kwanza wamecheza mechi 33.