RIVERS UNITED 0-0 YANGA

UBAO wa Uwanja wa Godswill Akpabio huko Nigeria unasoma Rivers United 0-0 Yanga ikiwa ni dakika 45 za awali.

Yanga inaliandama lango la wapinzani wao katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika wakimtumia Fisto Mayele na Aziz KI.

Mashuti 6 Yanga wamepiga matatu yamelenga lango huku Rivers wakiwa wamepiga mashuti 7 hakuna hata moja lililolenga lango.

Ni mchezo wa hatua ya robo fainali ya kwanza Kombe la Shirikisho Afrika.