Home Uncategorized SIMBA YAKUNJA MKWANJA WA M-BET M 100

SIMBA YAKUNJA MKWANJA WA M-BET M 100

WAKATI wachezaji wa Simba wakitarajia kuanza mazoezi leo Aprili 18,2023 kwa ajili ya mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Club Athletic ya Morocco, wadhamini wakuu wa timu hiyo, kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet Tanzania imekabidhi bonasi ya Sh milioni 100.

Wachezaji wa Simba walikuwa kwenye likizo fupi baada ya kibarua kigumu dhidi ya wapinzani wao,Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC na kushinda kwa mabao 2-0.

Baada ya kibarua hicho kigumu wababe hao wa Mtaa wa Msimbazi watakuwa wenyeji wa mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Wydad Club Athletic kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa unaotarajiwa kuchezwa kuanzia saa 10:00 jioni.

Akizungumza  wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi amesema kuwa wamefurahishwa na hatua ya klabu hiyo waliyofikia katika mashindano hayo na kuamua kuongeza morali kwa wachezaji.

Mushi amesema kuwa wanajivunia mafanikio waliyofikia klabu hiyo na wanaamini wataendelea kung’ara katika mashindano hayo.

Alieleza kuwa fedha hizo ni sehemu ya wajibu wao wa udhamini na wataendelea kuwapa bonasi kadri wanavyoendelea kufanya vizuri zaidi.

“Tunajivunia sana kwa mafanikio ya klabu katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.  Huu ni mwendelezo wa kufanya vyema kwani msimu uliopita walifanya vizuri pia katika mashindano ya Kombe la Shirikisho na kufikia hatua ya robo fainali.

“Hii ni sehemu ya makubaliano kwenye mkataba na tunaamini kwamba mmilioni 100 ni fedha ambazo tunawapa kadri wanavyozidi kufanya vizuri ndivyo ambavyo wanapata bonasi zaidi,” amesema Mushi.

Kwa upande wake,  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Imani Kajula amesema wapo tayari kukabiliana na mabingwa watetezi wa michuano hiyo na kuwataka mashabiki wa soka kuhudhuria pambano hilo.

Kajula amesema bonasi ya M-Bet  imeongeza morali kabla ya pambano hilo na wachezaji waliahidi kutowaangusha.

“Sisi ni klabu yenye heshima barani Afrika na tutaendelea kufanya vyema zaidi na kuwa moja ya  klabu kubwa katika bara letu. Mara zote tunaangalia vitu vikubwa katika na tunaamini tiutafikia malengo yetu,” amesema Kajula.

Katika hatua nyingine, wachezaji wa Simba wameanza maandalizi kuelekea mchezo wa Jumamosi.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wachezaji wawili, Sadio Kanoute na kipa chaguo la kwanza Aishi Manula ni miongoni mwa wachezaji waliojiunga na timu hiyo baada ya kuwa nje kutokana na majeraha.

Ally amesema wawili hao watachunguzwa afya zao kabla ya hatua nyingine.

Previous articleYANGA BADO WANA JAMBO LAO
Next articleVIDEO:MWAKINYO KUZICHAPA NA TWAHA/AFUNGUKIA ISHU YA SUMU