KOCHA Mkuu wa KMC,Jamhuri Khiwelu, ‘Julio’ amesema kuwa ana matumaini makubwa ya kuongeza ari kwenye mechi ambazo zimebaki.
Julio amechukua mikoba ya Hitimana Thiery ambaye alifikia makubaliano ya kuvunja mkataba na timu hiyo kutokana na mwendo mbovu.
Mchezo wa mwisho kwa Hitimana kukaa benchi alishuhudia ubao ukisoma KMC 0-2 Geita Gold.