Home Sports VINARA WA LIGI KUFANYIWA MAZOEZI MAALUMU

VINARA WA LIGI KUFANYIWA MAZOEZI MAALUMU

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa wachezaji wao wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Aprili 16 huku wachezaji wote wakiwa fiti.

Miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao hawakuwa fiti hivi karibuni ni Shomari Kapombe aliyepata maumivu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Raja Casablanca, Aishi Manula na Henock Inonga hawa walipata maumivu mchezo dhidi ya Ihefu ambao ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho.

 Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa tayari wachezaji wapo tayari kwa mchezo huo na watapambana kufanya vizuri kupata matokeo.

“Baada ya kukamilisha mchezo wetu dhidi ya Ihefu kikosi kimerejea Dar na wachezaji wamewasili kambini na jioni wataanza mazoezi maalumu kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Yanga.

“Wachezaji wetu wapo vizuri wote na hakuna majeruhi kwa wale ambao walipata majeruhi kwenye mchezo dhidi ya Ihefu wote wapo tayari na maendeleo yao ni mazuri,” amesema Ally.

Imani Kajula, Mtendaji Mkuu wa Simba amesema kuwa wanaamini mchezo huo utakuwa ni wa kipekee na mashabiki wengi watajitokeza uwanjani kushuhudia mchezo huo kutokana na utaratibu maalumu waliokuja nao kwenye uuzaji wa tiketi.

Previous articleVIGOGO SIMBA SC WAMFUNGIA KAZI NABI WA YANGA
Next articleWIMBO MPYA WA CHRIS JABARI SINA MASHAKA HUU HAPA