YANGA:HATUNA MASHAKA KIMATAIFA, TUPO TAYARI

ALI Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amebainisha kuwa hawana mashaka na hatua ya robo fainali waliyofikia zaidi ni hesabu kwenye mechi za hatua hiyo kupata matokeo chanya.

Yanga imakamilisha kundi D ikiwa ni namba moja kibindoni ilikusanya pointi 13 huku safu yake ya ushambuliaji ikiwa imetupia mabao 9.

Inakibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Rivers United baada ya kupangwa kwenye droo iliyochezwa jumatano, Misri na itaanzia ugenini na kumaliza kete ya pili Uwanja wa Mkapa.

Kamwe amesema kuwa kazi kubwa awali ilikuwa kutinga hatua ya robo fainali jambo ambalo limetimia hivyo hesabu zinahamia robo fainali.

“Kukamilisha malengo ya kucheza hatua ya robo fainali hii ni kubwa kwetu na sasa tupo katika hatua ambayo tulikuwa tunaifikira mwanzo na sasa hesabu ni kwenye mechi ambazo tutacheza hatua ya robo fainali.

“Hatuna mpinzani ambaye tunamuhofia kwani wachezaji wamekuwa imara na kila mmoja anatambua kwamba ili kufika hatua ya nusu fainali ni lazima kushinda mechi ya robo fanali.

“Rivers United ni timu bora ila kwa kuwa tunakutana nao basi tupo tayari kupata matokeo mazuri kwenye mechi zetu zote nyumbani na ugenini,”.

Timu hiyo kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya mwisho kuikabilia Geita Gold mchezo wa hatua ya robo fainali Kombe la Azam Sports Federation na miongoni mwa wachezaji waliopo kambini ni pamoja na Aziz KI, Bernard Morrison,Yannick Bangala.