MWENDO WA TP MAZEMBE NA YANGA WALIKIMBIZANA KWELI

  NJE ndani TP Mazembe kaacha pointi tatutatu mbele ya Yanga walipokutana kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi wote wakiwa kundi D.

  Yanga wamekamilisha mechi ya sita wakiwa wanaongoza kundi na kibindoni wana pointi 13, hapa tunakuletea kazi ilivyokuwa Uwanja wa TP Mazembe:-

  Lenny Junior

  Kipa huyu aliokoa hatari dakika ya 6,14,15 alipiga faulo dakika ya 46 huku akitunguliwa bao moja dakika ya 63.

  Christian Kwame

  Nyota huyu alikuwa kwenye kazi ngumu katika kutimiza majukumu yake dakika ya 28,43,29 alimwaga krosi kuelekea lango la Yanga.

  Luzoro Sita

  Ni dakika ya 11,12 alimwaga krosi alipiga faulo dakika ya 38 na dakika ya 47 shuti lake lililenga lango.

  Kouame

  Nahodha Christina Kouame ni shuhuda wa timu hiyo ikiambulia pointi tatu kwenye mechi sita huku ikifungwa nje ndani na Yanga yeye akiwa na kitambaa cha unahodha.

  Joel Beya

  Alimwaga krosi dakika ya 10,66 alicheza faulo dakika ya 32 akaonyeshwa kadi ya njano, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 61 na dakika ya 12 na 61 alipiga mashuti ambayo yalilenga lango.

  Alex Ngonga

  Bao pekee ambalo waliwafunga Yanga Uwanja wa Mkapa lilifungwa na mwamba huyu dakika ya 80. Shuguli yake kwenye mchezo wa Uwanja wa TP Mazembe ilikuwa nzito kwelikweli.

  Alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 7 alicheza faulo dakika ya 40,48 82 alionyeshwa kadi ya njano kama ilivyokuwa dakika ya 88 na kuonyeshwa kadi nyekundu, alirusha dakika ya 8 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 79.

  Metacha Mnata

  Aliokoa hatari dakika ya kwanza kisha kazi iliendelea dakika ya 6,12,14,17,42,43,45,47,60,61,71,89,90 alipiga faulo dakika ya 22.

  Moloko

  Jesus Moloko alipiga krosi dakika ya 6,7,40,63.

  Mudathir Yahya

  Muda alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 52, alipiga shuti lililolenga lango dakika ya 6 lile ambalo halikulenga lango ilikuwa dakika ya 18 huku akimwaga krosi dakika ya 31.

  Aliyeyusha dakika 54 nafasi yake ilichukuliwa na Farid Mussa ambaye alifunga dakika ya 63.

  Musonda

  Kennedy Musonda alipiga krosi dakika ya 6,16,45 alipiga faulo dakika ya 45 aliyeyusha dakika 80 aliingia Clemnt Mzinze.

  Bacca

  Ibrahim Abdalah, ‘Bacca’ aliokoa hatari dakika ya 10,28,31,42,43,45,46,49 alipiga krosi dakika ya 6,17 alicheza faulo dakika ya 21 alichezewa faulo dakika ya 26,32.

  Mayele

  Fiston Mayele alichezewa faulo dakika ya 82,88 alipiga krosi dakika ya 7,43 alicheza faulo dakika ya 40.

  Lomalisa

  Joyce Lomalisa alipiga krosi dakika ya 7,29,45,63 alipiga faulo dakika ya 11,51 aliokoa dakika ya 27.

  Bangala

  Yannick Bangala aliokoa hatari dakika ya 12,38,40,44 alichezewa faulo dakika ya 19,31,40,48.

  Bakari Mwamnyeto

  Aliokoa hatari dakika ya 14,16,21,31,31,53,58.

  Salim Aboubhakari

  Sure Boy alimwaga krosi dakika ya 14,19,45 alicheza faulo dakika ya 39,46 aliyeyusha dakika 65 akaingia Zawad Mauya.

  Job

  Dickson Job aliokoa hatari dakika ya 25,39,46,49,71 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 82 alichezewa faulo dakika ya 71.

  Matokeo ya Yanga kundi D

  Monastri 2-0 Yanga

  Yanga 3-1 Mazembe

  Bamako 1-1 Yanga

  Yanga 2-0 Bamako

  Yanga 2-0 Monastir

  TP Mazembe 0-1 Yanga

  Previous articleVIDEO:MO AFUNGUKIA USAJILI WA MAYELE WA YANGA
  Next articleROBO FAINALI CAF:WALETENI TUMALIZANE