TP Mazembe wametunguliwa mabao 4-1 dhidi ya Yanga wawakikilishi wa Tanzania,Kombe la Shirikisho Afrika.
Mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 3-1 TP Mazembe.
Mchezo wa pili Uwanja wa TP Mazembe ubao umesoma TP Mazembe 0-1 Yanga ikiwa ni hatua ya makundi.
Mtupiaji ugenini ni Farid Mussa dakika ya 63 na kuifanya Yanga kufikisha pointi 13 ikiwa namba moja katika kundi.