Home Sports GEITA GOLD WAIVUTIA KASI YANGA

GEITA GOLD WAIVUTIA KASI YANGA

WACHEZAJI wa Geita Gold chini ya Kocha Mkuu Fred Felix ‘Minziro’ wanaendelea na maandalizi kuelekea mchezo wao wa hatua ya robo fainali Azam Sports Federation.

Geita Gold watavaana na Yanga Aprili 8, 2023 katika dimba la Azam Complex Chamazi.

Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi wa taji hilo ni Yanga walioshinda dhidi ya Coastal Union.

Katika mchezo wao wa ligi walipokutana Uwanja wa Azam Complex Geita Gold ilipoteza pointi zote tatu mazima licha ya kuanza kupata bao kipindi cha kwanza.

Ubao ulisoma Yanga 3-1 Geita Gold baada ya dakika 90 kumeguka kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Previous articleMASTAA AZAM FC WAREJEA WAANZA KAZI
Next articleVIDEO:MWAKINYO HUYU HAPA MSIKIE KUHUSU PAMBANO LAKE