>

SIMBA KAMILI KUIKABILI RAJA CASABLANCA

ROBERTO Oliveira, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ameidaa vizuri timu kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa nchini Morocco Machi 31 saa 4:00 usiku kwa Afrika Mashariki hapa nyumbani Tanzania itakuwa ni Aprili Mosi saa 7:00 usiku.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye msafara huo ni pamoja na Gadiel Michael, Sadio Kanoute, John Bocco, Moses Phiri,Kennedy Juma na Joash Onyango.

Huo ni mchezo wa mwisho katika hatua ya makundi ambapo kwenye mchezo ule uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 0-3 Raja Casablanca.

“Nimeandaa timu kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Raja Casablanca na tunaamini kwamba utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani lakini tupo tayari kwa ajili ya ushindani,” amesema.

Raja haijapoteza mchezo kwenye hatua ya makundi na waliwatungua mabao 5-0 Vipers kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mohamed V hivyo Simba wanakazi kubwa ya kufanya mbele ya wenyeji hao ambao wanacheza mpira wa spidi na pasi nyingi.