KOCHA MAN U ANAMKUBALI MARTIAL

TEN Hag, Kocha Mkuu wa Manchester United ameweka wazi kuwa ana imani na mshambuliaji wake Anthony Martial.

Mshambuliaji huyo hajawa kwenye mwendo bora ndani ya timu hiyo lakini kocha amekubali kazi yake.

Nyota huyo mwenye miaka 27 amekuwa na msimu mbaya chini ya Ten Hag ambapo amekuwa na majeraha ya mara kwa mara akiwa amekosa mechi 30 kutokana na majeraha hayo.

Kuna hofu kuwa anaweza kuachwa msimu ujao kutokana na mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu.

“Sifikirii ni muda muafaka kulizungumzia hilo ninamuamini na kilamara atakuwepo amekuwa akijituma kwa ajili ya timu na hata ari ya timu inakuwa juu,”.