CHAMA KAMA CHAMA ANAKIMBIZA CAF

    CLATOUS Chama mwamba wa Lusaka kwenye mashindano ya kimataifa anafanya vizuri ikiwa ni nembo kwa wazawa kushtuka na kuiga namna anavyofanikiwa.

    Anaingia kwenye orodha ya wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa CAF mchezo wa tano akiwa na mshikaji wake Sadio Kanoute hawa wote wapo ndani ya Simba na ikumbwe kuwa kwenye mechi ya nne alisepa na tuzo hiyo alipoingia kwenye orodha kwa mara ya kwanza.

    Katajwa kwenye orodha ya wachezaji waliopo kwenye kikosi bora cha wiki kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na Kanoute, Kapombe na Jean Baleke hawa wote ni kutoka Simba.

    Chama ameingia kwenye orodha ya nyota 10 wafungaji bora wa muda wote kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

    Ni mabao 19 kafunga jumla raia huyo wa Zambia akipachika mabao hayo kwenye ligi hiyo kubwa iliyoanzishwa 1964.
    Ni mabao 15 kafunga akiwa na Simba huku manne akifunga akiwa na Zesco United ya Zambia.

    Msimu huu kapachika mabao matano akifunga matatu dhidi ya Horoya, moja dhidi ya Vipers na moja dhidi ya de Agosto kwenye raundi ya pili.

    Msimu wa 2021 Chama alitupia mabao matano ilikuwa dhidi ya Plateau United,AS Vita,FC Platinum na Kaizer Chiefs.

    2018/19 ni mabao matano ilikuwa dhidi ya Mbabane Swallows,Nkana na AS Vita huyu ndiye Chama yupo Zambia kwa sasa kwenye majukumu ya timu ya taifa.

    Previous articleYANGA YAINGIA CHIMBO KUSAKA STRAIKA,SIMBA WANAITAKA FAINALI
    Next articleVIDEO:JEMBE AFUNGUKIA KAMBI YA STARS