NABI KUMALIZA MCHEZO MAPEMA KWA WAARABU

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kuna nguvu kubwa kwa wachezaji kupata matokeo mapema jambo linaoongeza nguvu ya kujiamini na kucheza kwa utulivu.

Timu hiyo inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa hatua ya makundi inasaka pointi tatu ili kufikisha malengo ya kutinga hatua ya robo fainali ina pointi 7 kwenye kundi D baada ya kucheza mechi nne.

Kituo chake kinachofuata ni dhidi ya US Monastri mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 19 wakiwa wanakumbuka kuwa walipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0.

 Nabi amesema kuwa kuna ugumu kwenye mashindano ya kimataifa kutokana na kila timu kuhitaji ushindi hivyo watajitahidi kupata matokeo mapema kuongeza nguvu ya kujiamini.

“Ikiwa tunakutana na timu imara ambayo inahitaji matokeo ni lazima tufanye kazi kubwa kwenye kutumia nafasi hasa zile za mwanzo zitatufanya tuwe imara na kupata matokeo mazuri.

“US Monastri ni timu imara ina wachezaji wazuri hata wachezaji wetu nao ni wazuri hivyo makosa ambayo tulifanya kwenye mchezo uliopita tunayafanyia kazi,” amesema Nabi.