Home Sports TUZO YAMPA NGUVU MUSONDA APANIA KUENDELEA KUTUPIA

TUZO YAMPA NGUVU MUSONDA APANIA KUENDELEA KUTUPIA

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Keneddy Musonda amepata fursa ya kupokea zawadi ya medali kutoka kwa mtoto Lucas Gomez Usoz kutoka Spain huku akiahidi kwamba ataendelea kufunga kila anapopata nafasi.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 8 anayeishi mjini Madrid nchini Spain alituma Medali hiyo kupitia ubalozi wa Spain (TZ) na kukabidhiwa rasmi leo na Balozi Jorge Moragas mbele ya Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hers Said kama sehemu ya kuvutiwa na uchezaji wa mshambuliaji huyo.

Musonda amesema kwake ni furaha kupewa tuzo hiyo na ataendelea kufanya vizuri akiwa na Yanga katika kutimiza majukumu.

“Ninafurahi kwa kupata zawadi na nitaendelea kufanya vizuri kwa ajili ya kutimiza majukumu yangu kwenye mechi zote na ninaamini nikipata nafasi nitafunga,”.

Hiyo yote ni baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi akiwa anaitumikia klabu yake ya zamani ya Power Dynamos FC ya nchini Zambia.

Hafla fupi iliyoandaliwa na balozi ilifanyika kwenye makazi yake eneo la Oyster bay, jijini Dar es salaam.

Jana Uwanja wa Azam Complex Musonda alikuwa miongoni mwa nyota waliopelea maumivu Geita Gold wakati ubao uliposoma Yanga 3-1 Geita Gold.

Previous articleKIKOSI CHA STARS AFCON HIKI HAPA,MBWANA, FEI NDANI
Next articleAZAM FC WAPEWA KIKOMBE CHAO MBEYA