Home Sports AZAM FC WAPEWA KIKOMBE CHAO MBEYA

AZAM FC WAPEWA KIKOMBE CHAO MBEYA

KIKOMBE ambacho Azam FC waliwapa Ihefu kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara nao wamekipokea vilevile ugenini.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Azam FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 huku mtupiaji akiwa ni Prince Dube muuaji anayetabasamu.

Machi 13,2023 ubao wa Uwanja wa Highland huko Mbeya umesoma Ihefu 1-0 Azam FC mtupiaji akiwa ni Rafael Loth.

Mapema mchezo uligota mwisho kwa Ihefu kupachika bao dakika ya 38 jitihada za Azam FC yenye Abdul Suleiman,’Sopu’ , Prince Dube kusepa na pointi ugenini ziligonga mwamba.

Azam FC inagotea na pointi zake 47 ikiwa nafasi ya nne huku Ihefu wao wakiwa nafasi ya 6 na pointi 33 kibindoni wote wamecheza mechi 25.

Previous articleTUZO YAMPA NGUVU MUSONDA APANIA KUENDELEA KUTUPIA
Next articleYANGA YATEMBEZA BONGE LA MKWARA KWA WAARABU