MPANGO kazi wa Kocha Mkuu wa Singaida Big Stars, Hans Pluijm kusepa na pointi tatu dhidi ya Coastal Union ulikwama baada ya kuambulia pointi moja.
Ikiwa ugenini baada ya dakika 90 Machi 12,2023 ubao wa Uwanja wa Mkwakwani ulisoma Coastal Union 1-1 Singida Big Stars.
Ni mastaa wawili walipachika mabao kwenye mchezo huo ambapo kwa Coastal Union wao ni Greyson Gerald alipachika bao dakika ya 44.
Mwamba Bright Adjei aliweka mzani sawa dakika ya 74 na kuwafanya Singida Big Stars kusepa na pointi moja ugenini.
Matokeo hayo yanaifanya Singida Big Stars kufikisha pointi 48 huku wakiwa nafasi tatu na Coastal Union nafasi ya 13 pointi 26.