Home Sports KOCHA WA SIMBA KUWAFANYIA SAPRAIZ HOROYA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

KOCHA WA SIMBA KUWAFANYIA SAPRAIZ HOROYA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

ROBERTO Oliveira ‘Robertinho’, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kila mchezo atafanya mabadiliko kulingana na mbinu za wapinzani wake anaokutana nao.

Timu hiyo ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa imetoka kushuhudia ubao wa Uwanja wa Manungu ukisoma Mtibwa Sugar 0-3 Simba.

Kwenye mchezo huo Robertinho alianza na washambuliaji wawili ambao ni Moses Phiri na Jean Baleke huku akimpa muda pia mshambuliaji wake Mohamed Mussa ambaye alitokea benchi kwenye mchezo huo.

Mchezo dhidi ya Horoya unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 18 ambapo Simba wanakumbuka walipoibukia Guinea walipoteza kwa kutunguliwa bao moja. Kwenye msimamo wa kundi C la michuano hiyo Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi sita vinara ni Raja Casablanca wenye pointi 12.
Kocha Mkuu wa Simba, Robertinho (kulia) akiongea na wachezaji wake.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Robertinho alisema kuwa wana kazi kubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika mashindano ambayo siyo mepesi lakini wanahitaji matokeo mazuri.

“Kila mchezo ambao tunacheza tunakuwa na mpango kazi maalumu ambapo tunahitaji kushinda na kufunga kwa kuwatumia wachezaji ambao tunao ukizingatia kwamba wengi wana vipaji na wanapambana kutafuta matokeo.

“Hakuna ambaye hatambui ubora wa wapinzani wetu ikiwa ni pamoja na Horoya, lakini nao ni lazima tuwe na mpango kwa ajili ya kuwakabili na kuwabadilishia mipango kulingana na namna ambavyo tutakutana nao hasa kwenye sehemu ya mazoezi hapo ndipo tunafanyia kazi makosa yetu,” alisema Robertinho.

Previous articleMECHI YA KISASI LEO
Next articleSINGIDA BIG STARS NGOMA NZITO NA COASTAL UNION