MECHI YA KISASI LEO

WABABE wawili leo wanatarajiwa kuvuja jasho ndani ya dakika 90 kusaka pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa ligi.

Ni Ihefu itawakaribisha Azam FC kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Highland Estate.

Kila timu itaingia kwa hesabu za kusaka pointi tatu na kuandika rekodi mpya ambapo Ihefu wao wanahitaji kulipa kisasi cha kutunguliwa mchezo wa mzunguko wa kwanza na  Azam FC wao hesabu zao ni kusepa na pointi tatu kwa mara nyingine tena

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao wa Azam Complex ulisoma Azam FC 1-0 Ihefu na mtupiaji akiwa ni Prince Dube dakika ya 54.

Kwenye mchezo huo ni Juma Nyoso wa Ihefu akionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 43.

Peter Andrew Ofisa Habari wa Ihefu amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Azam FC yapo tayari huku Azam FC chini ya Kocha Mkuu Kali Ongala nao wakibainisha kuwa wanahitaji pointi tatu.