YANGA imeibuka na ushindi kwenye mchezo wake wa ligi dhidi ya Geita Gold ikiwa ni mzunguko wa pili.
Ubao wa Uwanja wa Azam Complex umesoma Yanga 3-1 Geita Gold.
Ni Geita Gold wao walianza kupachika bao la kuongoza mapema kipindi cha kwanza dakika ya 19 kupitia kwa Elias Maguli ambalo lilidumu mpaka muda wa mapumziko.
Kipindi cha pili Yanga walianza kwa kasi kupitia kwa Kennedy Musonda dakika ya 48 na Clement Mzize na dakika 50.
Moloko ni dakika ya 70 alipachika bao hilo kwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.