Home Sports IHEFU KAMILI KUIKABILI AZAM FC

IHEFU KAMILI KUIKABILI AZAM FC

KOCHA wa Ihefu Temy Felix amesema kuwa wanatambua mchezo wa kesho dhidi ya Azam FC utakuwa mgumu lakini wanahitaji matokeo mazuri.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Azam FC 1-0 Ihefu na kuwafanya wayeyushe pointi tatu.

“Mchezo muhimu kwetu na tunatambua utakuwa na upinzani mkubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwa pamoja nasi kila kitu kitakuwa sawa,”

Pia kwenye mchezo huo ni Juma Nyoso alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea faulo nyota wa Azam FC.

Joseph Mahundi nahodha wa Ihefu amesema wapo tayari kwa mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Highland Estate.

Previous articleVIDEO:NYOMI LA MASHABIKI WA YANGA MAKAO MAKUU
Next articleHIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA GEITA GOLD