Home Uncategorized SIMBA INAAMINI ITAPATA UGUMU KWA MTIBWA

SIMBA INAAMINI ITAPATA UGUMU KWA MTIBWA

JUMA Mgunda, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa wanatambua watapata upinzani mkubwa kwenye mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar.

Simba itakuwa Uwanja wa Manungu kusaka pointi tatu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao nao wanazihitaji pia.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 5-0 Mtibwa Sugar.

Mgunda amesema:”Tunategemea kupata ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wetu lakini tunahitaji pointi tatu.

“Maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar yapo tayari na tunatambua kwamba itakuwa kazi kubwa, wachezaji wapo tayari na tutapambana kupata matokeo,” amesema.

Machi 10 wachezaji wa Simba walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa leo ambapo miongoni mwao ni pamoja na Shomari Kapombe, Sadio Kanoute, Aishi Manula, Clatous Chama.

Previous articleKMC YAVUNJA REKODI MBOVU YASHINDA KWA MARA YA KWANZA
Next articleVIDEO:IKIJIANDAA KUIVAA GEITA GOLD MASTAA HAWA YANGA KUKOSEKANA