KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ameweka wazi kuwa hakufurahishwa tabia ya ubinafsi iliyokuwa ikifanywa na mshambuliaji wa timu hiyo, Fiston Mayele licha ya kumuweka chini ya kumueleza juu ya jambo hilo.
Nabi ametoa kauli hiyo kufuatia mshambuliaji huyo kulazimisha kufunga mwenyewe katika nafasi alizokuwa anapata licha ya kutokuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga katika mchezo wa juzi dhidi ya Real Bamako ya Mali ukiwa ni wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar na Yanga kushinda 2-0 mabao yakifungwa na Mayele na Jesus Moloko.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Nabi alisema kuwa amelazimika kumueleza mshambuliaji huyo juu ya ubinafsi wa kulazimisha kufunga yeye katika mchezo huo hakuwa ni kitu kizuri kutokana na wao kutafuta ushindi wa timu na siyo wa mtu mmoja.
“Haikuwa kitu kizuri katika timu na nilimueleza wakati wa mapumziko kwamba hakufanya jambo zuri la yeye kulazimisha kufunga licha ya kutokuwa katika nafasi ya nzuri lakini alieleza kwamba hakusikia wakati wenzake walipokuwa wakiomba mpira.
“Lakini nitaongea na wachezaji wote katika eneo la mazoezi kwa sababu nataka watambue wazi kwamba tunachokifanya ni juu ya suala kutafuta ushindi wa timu na siyo wa mtu mmoja hivyo hatupaswi kucheza kwa ubinafsi wa aina yoyote kwa maana tunafuata malengo ya timu kuweza kufikia,” alisema Nabi.
MSIMAMO WA YANGA CAF
P W D L GF GA
1.US Monastir 4 3 1 0 6 1 10
Yanga 4 2 1 1 6 4 7
3.TP Mazembe 4 1 0 3 4 7 3
4.Bamako 4 0 2 2 3 7 2