Home Sports MITAMBO YA KAZI SINGIDA BIG STARS KAMILI GADO

MITAMBO YA KAZI SINGIDA BIG STARS KAMILI GADO

HALI ya nyota wa Singida Big Stars, Bruno Gomez inazidi kurejea taratibu kwenye ubora wake baada ya kupata maumivu hivi karibuni.

Nyota huyo ambaye ni mtaalamu wa mapigo huru akiwa amewapa tabu makipa waliopo ndani ya tatu bora ikiwa ni Azam FC na Simba alipata maumivu ya miguu kwenye mazoezi.

Mbali na Bruno raia wa Brazil pia mwamba mwingine ambaye naye ameanza kurejea kwenye ubora ni Yassin Mustapha.

Mustapha alikuwa alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya misuli jambo lililofanya asiwe fiti kupambania nembo ya timu hiyo ya Wakulima wa Alizeti.

Kwenye msimamo Singida Big Stars ipo nafasi ya 4 ikiwa imekusanya pointi 47 baada ya kucheza mechi 24.

Ni mabao 28 timu hiyo imefunga huku kinara wao wa utupiaji akiwa ni Bruno mwenye mabao 9 kibindoni.

Previous articleMASHINE MPYA YA KAZI YATUA YANGA
Next articleMASHABIKI MNASTAHILI PONGEZI,WACHEZAJI KAZI IPO