Home Sports MASHINE MPYA YA KAZI YATUA YANGA

MASHINE MPYA YA KAZI YATUA YANGA

WAWAKILISHI kwenye anga za kimataifa katika Kombe la Shirikisho Yanga Machi Mosi wamemtambulisha Khalil Ben Yousef raia wa Tunisia ambaye ni mtaalamu wa kusoma mipango ya timu pinzani na mifumo yao pamoja na viwango vya wachezaji wa Yanga.

Mtaalam huyo amewahi kufanya kazi katika timu kubwa kama Esparence de Tunis na Timu ya Taifa Tunisia katika madaraja yote.

Amefanya kazi hiyo kwenye ngazi ya timu za vijana na timu za wakubwa.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi akishirikiana na Cedrick Kaze kesho Machi 3 ina kibarua kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex hivyo Yanga wameongeza wataalamu kwenye benchi lao la ufundi.

Previous articleMAYELE AFICHUA MAGUMU YA CAF,PHIRI ATOA AHADI NZITO
Next articleMITAMBO YA KAZI SINGIDA BIG STARS KAMILI GADO