CHELSEA IMEBUTULIWA HUKO

TOTTENHAM imesepa na pointi tatu muhimu katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea.

Mabao ya Oliver Skipp dakika ya 46 na Harry Kane dakika ya 82 yameipa ushindi Spurs.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Tottenham Hotspur umesoma Tottenham 2-0 Chelsea.

Chelsea inabaki na pointi 31 ikiwa nafasi ya 10 huku Tottenham ikifikisha pointi 45 nafasi ya nne.