Home Sports KINYOZI MUSOMA ALAMBA 6,776,051 JACKPOT BONUS YA SPORTPESA

KINYOZI MUSOMA ALAMBA 6,776,051 JACKPOT BONUS YA SPORTPESA

Mkazi wa Musoma, Mara Mwaliki Maregeli Nyangasi ameshinda
kitita cha Sh 6,776,051 kama Jackpot bonus ya kati kati ya wiki baada ya kupatia kwa usahihi mechi 12 kati ya mechi 13 za Jackpot zilizochezwa wiki iliyopita.

Akizungumza katika ofisi za SportPesa, Oysterbay,Dar-Es-Salaam,
Mwaliki anasema alianza kucheza na SportPesa 2017, baada ya
kusikia na kuona kwenye magazeti washindi waliokuwa
wakitangazwa baada ya kushinda.

“Mimi nilianza kucheza rasmi na SportPesa miaka mitano iliyopita baada ya kuwa mara kwa mara naona matangazo kwenye kurasa za mtandao na pia kwenye magazeti baadhi ya washindi ambao walikuwa wanawekwa mule.

Akindelea Mwaliki anasema haikuwa rahisi kwa yeye kutoboa mpaka wiki iliyoisha ndipo kwa mara ya kwanza ameshinda kitita kinono tangu ameanza kucheza michezo ya kubashiri na SportPesa.

“Unajua mimi sikukata tamaa hata baada ya kuwa sikuwahi kushinda mahela kama wengine walivyokuwa wanashinda. Kikubwa niliweka imani ipo siku ninaweza kufanikiwa na sasa ndio nimeanza kuona dalili.

“Mimi ninajitahidi sana kufukuzia ile bilioni 1, na vile vile nikipata
muda nacheza pia Jackpot hii ya katikati ya wiki na namshukuru
Mungu na mimi nimeweza kubahatika kushinda mechi 12 na kupata bonus ya Sh 6,776,051.

Akizungumzia ni kwa namna gani alicheza mkeka wa Jackpot ya katikati ya wiki ambao ameshinda Mwaliki anasema yeye kwa wiki huwa anaweka mikeka ya Jackpot mara 2 tu.

“Mimi huwa nacheza Jackpot ya kati kati ya wiki kila siku ya  Jumatano na Supa Jackpot kila siku za mwisho wa wiki.

“Kwa mfano mkeka huu niliyoshinda niliuweka siku ya Jumatano
asubuhi na kusubiria matokeo bila kuwa nafuatilia mechi. Kwa bahati nzuri nimeshinda mechi 12 na kujishindia Jackpot bonus hii iliyonileta hapa ofisi za SortPesa.

Mwaliki anamalizia kwa kuwataka Watanzania kutokata tamaa na
kuendelea kuamini katika ndoto zao, kwani hakuna anayejua siku
yake itafika lini.

“Niwaase tu Watanzania wenzangu kuamini kile
ambacho unapenda kukifanya. Huwezi jua siku yako ni lini, hivyo
nawaasa kutumia fursa hii ya SportPesa kucheza na kushinda kama mimi,” .

Akitoa neno la hongera kwa mshindi Mkuu wa kitengo cha
Mawasiliano kampuni ya SportPesa Sabrina Msuya amesema kampuni wamedhamiria kuwawezesha kwa namna ya kipekee
ambapo wateja wanashinda zawadi mbali mbali baada ya
kucheza Jackpot, mechi za multibet, Single bet, Kasino, michezo
ya Virtual na michezo mingine mingi.

“Niwakumbushe tu watanzania kama ambavyo nimekuwa nikisema kila tunapopata washindi wa Jackpot bonus Watanzania waendelee kuiamini SportPesa kwa kuwa malipo ni papo hapo na washindi wanashinda kila siku na kila wiki kama ambavyo Japhet Msangawale wa Rukwa,Sumbawanga alivyoshinda wiki iliyopita Sh 248, 672,790,”

Wiki hii Supa Jackpot imesimamia 1,080,318,061.

Previous articleMANCHESTER UTD VS FC BARCELONA KUKIWASHA LEO LIGI YA UROPA BARANI ULAYA
Next articleWAARABU WAIBEBA YANGA MALI, PHIRI AVALISHWA MABOMU AWALIPUE VIPERS