RUVU SHOOTING INAPAMBANA KUREJEA KWENYE UBORA

UONGOZI wa Ruvu Shooting umeweka wazi kuwa kwa sasa unapambana na hali waliyonayo kurejea kwenye ubora.

Timu hiyo haijawa kwenye mwendo mzuri kutokana na kushindwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi za ligi.

Mchezo wake uliopita ilipoteza pointi tatu kwa kufungwa mabao 3-2 dhidi ya Geita Gold, Uwanja wa Nyankumbu mchezo wao ujao ni dhidi ya Kagera Sugar.

 Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema kuwa wanapambana na hali zao kwenye mechi zijazo ili kuwa bora.

“Ni kweli hatujawa na matokeo mazuri kwenye mechi ambazo tunacheza lakini haina maana kwamba mpapaso utakuwa umefika mwisho bado kazi ipo.

“Wachezaji wanaendelea kuimarika na kwa mechi zinazokuja tuna amini kwamba tutapata matokeo kikubwa ni kuzidi kuwa pamoja na hilo litatufanya tuwe imara,” amesema Bwire.