BARCELONA NA MAN U NGOMA NZITO

NGOMA ilikuwa ni nzito kwenye mchezo wa Europa League baada ya wababe wawili kutoshana nguvu kwenye mchezo huo.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Cam Nou ulisoma Barcelona 2-2 Manchester United.

Ni mashuti 18 timu zote mbili zilipiga kuelekea kwenye lango la wapinzani wao huku Barcelona wao mashuti 8 yakilenga lango alilikuwa Degea huku United wakipiga mashuti matano ambay yalilenga lango.

Kwa upande wa kona ni 8 zilipigwa kwa Barcelona huku Manchester United wao wakipiga jumla ya kona tano kwenye mchezo huo.

Mabao ni mali ya Marcos Alonso dakika ya 50 na Raphina dakika ya 76 kwa upande wa Barcelona.

Yale ya Manchester United ni mali ya Marcus Rashford dakika ya 62 na lile la pili ni mali ya Jules Koundes ambaye alijifunga dakika ya 59.