ROBERTINHO: SAIDO KARUDI, RAJA HAWATOKI
KOCHA wa Simba, Mbrazil Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amefunguka kuwa, watakuja kuzifunga timu zote kwenye Uwanja wa Mkapa wakianza na Raja Casablanca kwa kuwa wachezaji wake muhimu akiwemo Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ watakuwa fiti. Robertinho ameweka wazi kuwa, kilichowafanya wafungwe kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya wakiwa ugenini ni kukosa bahati…