KIMATAIFA VITENDO VINAHITAJIKA KUKAA KIMYA MWIKO

    KUKAA kimya ni jibu gumu ambalo linaleta maumivu kwa wale ambao wanakutegemea na kukuamini hivyo ni lazima uongee kwa namna yoyote ile.

    Kwenye ulimwengu wa michezo kwenye anga la kimataifa kukaa kimya kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi ni kukosa kutumia nafasi jambo linalofanya kila mmoja kupata maumivu.

    Ni kazi ngumu na kubwa kwa wawakilishi wa Tanzania ambayo wanayo kwa sasa ambayo ni kusaka ushindi ili waongee kwa vitendo na sio kukaa kimya.

    Muda ule wa kukaa kimya ilikuwa wakati ule wa maandalizi tayari umegota mwisho ni mwendo wa matokeo kwenye mechi za nyumbani na ugenini.

    Ukweli ni kwamba wachezaji wanahitaji kushinda hata wapinzani wanahitaji ushindi ni muda wa kuendelea kupambana hata matokeo yanapokuwa magumu kwenye mechi zenu.

    Simba ni kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga ikiwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika na zote zimetinga hatua ya makundi itapendeza ikiwa zitahama kwenye hatua hiyo na kusonga mbele.

    Hatua inayofuata ni kwenye hatua ya robo fainali ambayo ni kubwa na inaongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji.

    Benchi la ufundi ni muhimu kufanya kazi kubwa kwenye kutengeneza mbinu ambazo zitawafanya wafanikiwe kushinda mechi zijazo.

    Kuna tofauti kati ya ligi na mechi za kimashindano ambapo huku ni mwendo wa mbinu kila timu inacheza kulingana na mbinu.

    Wawakilishi wetu kimataifa kila la kheri kwenye kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.

    Previous articleSloti ya Pirates Power Ndani ya Meridianbet Ushindi ni Rahisi!
    Next articleVIDEO:KUMBE YANGA WAMEFANYIWA FIGISU