SIMBA TAYARI KUIKABILI HOROYA KIMATAIFA

JUMA Mgunda,kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa maandalizi yote kuhusu mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya ya Guinea yamekamilika.

Leo wawakilishi hao wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wanakibarua cha kusaka pointi tatu ugenini mchezo wa hatua ya makundi ambao ni wa kwanza kila timu.

Mgunda ameweka wazi kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa lakini wapo tayari.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa kimataifa dhidi ya Horoya, wapinzani wetu ni wazuri nasi tunatambua hilo tunawaheshimu huku tukiwa tunahitaji kupata matokeo mazuri,”

Kikosi hicho kipo nchini Guinea kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kwa mchezo huo utakaochezwa Fenruari 11 na Februari 10 walifanya mazoezi ya mwisho.

Miongoni mwa nyota ambao wapo tayari kuikabili Horoya ni Ally Salim, Beno Kakolanya na Aishi Manula kwa upande wa makipa wengine ni Mzamiru Yassin, Kibu Dennis, Henock Inonga.