KIMATAIFA INAWEZEKANA KAZI KUBWA IFANYIKE

  HAKIKA kwa sasa mambo yamezidi kupamba moto kwenye anga za kimataifa ambapo leo Simba wana kazi yakufanya kwenye anga za kimataifa

  Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kazi yao ni kwenye mchezo wa makundi ikiwa ni dhidi ya HoroyaAC hautakuwa mchezo mwepesi wala mgumu muhimu maandalizi mazuri.

  Kwa wachezaji kazi yenu iwe moja kusaka ushindi bila kuogopa kwenye mchezo wa leo huku mkitimiza majukumu yenu kusaka kufikia malengo ambayo mmejiwekea.

  Mashabiki dua zenu ni muhimu hasa ukizingatia ni wakati ambao kila mmoja anapenda kuona timu inashinda na kusonga mbele kwenye anga za kimataifa.

  Hii ni kazi kubwa ambayo kila mmoja anapaswa kuifanya wakati huu kuendelea kuiombea mema timu yake hili ni jambo la kila mmoja.

  Yanga nao wana kibarua kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ambapo wana kazi yakufanya kwenye mchezo dhidi ya US Monastri, timu hii nayo sio ya kubeza.

  Kila mmoja anatambua kwamba kufanya vizuri kwa wawakilishi wa Tanzania kimataifa ni furaha kwa kila mmoja huku wachezaji wakiongeza thamani yao kwenye kazi ambayo wanafanya.

  Muda huu wawakilishi wa Tanzania maandalizi ya mwisho mazuri ni muhimu na kila mmoja afanye kazi kwa umakini kutimiza majukumu yake.

  Kwenye mechi zote muhimu kucheza kwa umakini bila kuhofia wapinzani licha ya kwamba mtakuwa ugenini, inawezekana na kila la kheri.

   

  Previous articleMECHI ZOTE KALI ZA WIKIENDI HII EPL, SERIE A, LA LIGA, BUNDASLIGA NA LIGUE 1
  Next articleSIMBA TAYARI KUIKABILI HOROYA KIMATAIFA