Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mhe. Jerry William Silaa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akichukua mikoba ya Nape Moses Nnauye ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Kabla ya uteuzi huu Mhe. Silaa alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.