SIMBA KAMILI KUIKABILI HOROYA KIMATAIFA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa utapambana kupata matokeo kwenye mchezo wao dhidi ya Horoya ambayo ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo wa hatua ya makundi unatarajiwa kuchezwa Jumamosi hii ya Februari 11, 2023 nchini Guinea.

Tayari kikosi cha Simba mapema alfajiri ya leo kilikwea pipa kuwafuata wapinzani wao kikiwa na wachezaji wake ikiwa ni pamoja na Jean Baleke, John Bocco, Habib Kyombo, Kibu Dennis na Moses Phiri kwa upande wa washambuliaji.

Ahmed Ally, Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa maandalizi yapo tayari na watakwenda kupeperusha bendera ya Tanzania ugenini kwa umakini.

“Tunatambua ushindani mkubwa lakini tupo tayari wachezaji na benchi la ufundi wanajua umuhimu wa mchezo huu,”.